BOBAN HUYOOO KWA WAGOSI WAKAYA
8th April 2013
B-pepe
Chapa
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam, Boban ambaye yuko nje ya kikosi cha Simba kwa zaidi ya mwezi sasa, amefikia maamuzi hayo baada ya kutofautiana mambo mbalimbali na uongozi wa Simba. Hata hivyo, kiungo huyo atalazimika kusubiri hadi msimu ujao ili kuichezea timu hiyo mpya.
Chanzo kiliiambia NIPASHE kuwa mbali na Boban, chipukizi wengine watatu nao wako katika mazungumzo ya kujiunga na timu nyingine za Ligi Kuu ya Bara kutokana na kuahidiwa mishahara minono tofauti na wanayolipwa sasa katika klabu hiyo ya Msimbazi.
Hata hivyo, Boban alipotafutwa na gazeti hili mchana alikataa kuzungumza chochote na kueleza kwamba anakula na atafutwe baadaye.
Mara ya pili alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi nyota huyo aliyewahi kuichezea Coastal Union kabla ya kujiunga na Simba hakupatikana tena.
Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Aurora, aliliambia gazeti hili kuwa bado timu yake haijapanga ni wachezaji gani itawasajili kwa msimu ujao.
Kiongozi huyo alisema kuwa ni mapema mno kusema lolote kipindi hiki ambacho ligi iko kwenye hatua za lalasalama.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage alisema kwamba Coastal hawajawafuata kuhusu suala la Boban.
Boban, kipa na nahodha Juma Kaseja pamoja na beki Amir Maftah ni baadhi ya wachezaji wa Simba ambao mikataba yao inamalizika mwisho mwa msimu huu.

Comments
Post a Comment