HABARI YA PINDA KUWASHA MOTO KWENYE MACHIMBO YA MORAMU ARUSHA
Waziri Mkuu Pinda wakati alipokuwa akitoa salamu za pole kwenye
uwanja wa kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa Mount Meru, ambako majeneza
13 yalikuwa zimeshaandaliwa tayari kwa mazishi na baadaye kutembelea
eneo la machimbo.
Alisema mchimbo hayo yaliyosababisha vifo vya watu 13 na majeruhi
wawili, yamesitishwa kwa muda, ili wataalam kuangalia uwezekano wa
kutathimini eneo hilo na kisha yatafunguliwa, ili yaendelee kutoa ajira
kwa vijana.
“Hatuwezi kuyafunga moja kwa moja sababu haya yanategemewa sana na
wakazi wa Arusha na pia ni eneo moja muhimu kwa ajira kwa vijana wetu,
muhimu kuweka mazingira salama,” alisema.
Aidha, alipongeza uongozi wa jiji, viongozi wa vyama vya siasa na
dini, kwa kuweza kuhakikisha miili ya marehemu inasitiriwa vizuri na
kuzikwa kwa taratibu zote.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema watu 15 ndio
waliopata maafa hayo, lakini kati yao 13 walifariki baada ya na mmoja
aitwaye Maliek Lenanu (40) amelazwa hospitali ya Mount Meru baada ya
kuangukiwa na jiwe kifuani na kufunikwa na mchanga hadi juu ya kifua.
Majeruhi huyo amweleza Waziri Mkuu Pinda, kwamba anamshukuru Mungu kwa kuokolewa.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliwapongeza
viongozi wa jiji la Arusha kwa kujitahidi kuokoa roho za marehemu hao,
lakini ilishindikana kuokoa uhai na kufanikiwa kupata miili yao.
Marehemu hao ni Japheti Neilyang, Gerald Neilyang, Japhet Raphael,
Elibariki Loserian, Fabian Bambo, Fred Loserian, Elias Fanuel, Wilbrart
Raphael, Christopher Kawishe, Gerald Masai, Julus Pallangyo, Gerald
Jacob na Alex Maliaki.
Majeruhi mmoja ambaye hakutajwa jina alitibiwa juzi na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Simanzi na vilio vilitawala hospitalini hapo baada ya majeneza hayo
kuwekwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti na kisha kuombewa na
viongozi mbalimbali waliohudhuria sala hiyo na wanandugu kuchukua miili
ya kila mmoja na kwenda kuzika.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa Mkoa wa Arusha, viongozi wa dini pamoja na wafuasi wa vyama mbalimbali.

Comments
Post a Comment