HABARI YA POLISI KUKAMATA MAJAMBAZI 25 KINONDONI
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela.
.
Watuhumiwa hao walikamatwa katika wiki ya kuelekea sikukuu ya
Pasaka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, pia wamekuwa wakifanya
uhalifu katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya
jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam,
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela, alisema baadhi ya
matukio ya wizi wanayofanya wahalifu hao ni pamoja na kukata vyavu za
madirisha na kuiba simu kwa kutumia ndoano iliyofungwa kipande cha wavu
wa chandarua.
Alisema baadhi ya waalifu hao, hutumia mbinu ya kukata makufuli na
makomeo ya milango kwa kutumia mikasi maalumu na kufanikiwa kuingia
ndani na kufanya vitendo vya uhalifu.“Jeshi la Polisi liliimarisha
ulinzi na usalama katika mkoa wa Kinondoni kwa kufanya doria na misako
katika maeneo yote na hatimaye tukafanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao,
na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi
kukamilika,” alisema Kenyela.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa huo limefanikiwa kukamata silaha aina ya
Shortgun mbili zenye namba, AB 44736 na 10883 pamoja na risasi 17
maeneo ya Kigogo baada ya wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
Pia walifanikiwa kukamata bastola aina ya Glock 19 yenye namba LZB
642 na TZ CAR 98189 ikiwa na risasi 12 na ganda moja tupu maeneo ya
Mabibo kufuatia msako mkali uliofanyika baada ya kutokea kwa tukio la
wizi maeneo ya Msasani.

Comments
Post a Comment