ILE HABARI YA MWANAJESHI KUUA DEREVA WA BAJAJ DAR HII HAPA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.
Askari anayedaiwa ni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  anadaiwa kuua dereva wa bajaj kwa kutumia bunduki katika maeneo ya Kawe Shoko, jijini Dar es Salaam.

Tukio la kuuawa kwa kijana huyo jana jioni inadaiwa lilitokana na  kutokea  mabishano kati yake na mwanajeshi huyo wakati ikipita eneo ambalo raia hawaruhusiwi kupita.

Vurugu kubwa zilitokea katika eneo hilo baada ya kutio hilo huku vijana wenzake marehemu kukusanyika kuhoji sababu za kuawa kwa mwenzao.

Mashuhuda walisema kuwa baada ya askari kuho kumpiga risasi kijana huyo na kumuua, mwili wake ulichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Mwandishi wa jamiileotz.blogspot.com alipofika eneo hilo majira ya saa 2:15 usiku, alikuta wananchi wakikimbia hovyo na huku milio ya risasi ikisikika.

Akizungumza na jamiileotz.blogspot.com kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,  Charles Kenyela, aluthibitisha  alikiri kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa bado Jeshi la Polisi linafuatilia ili kupata taarifa zaid

Comments

Popular Posts