MAAJABU WATOTO 54 WAZALIWA KWENYE SKUKUU YA PASAKA MOROGORO
Baadhi ya wakinamama waliojifungua siku ya Pasaka wakiwa na watoto wao.
Kati ya watoto hao waliozaliwa kuanzia Ijumaa Kuu, siku ya kuteswa
kwa Yesu Kristo na kufufuka kwake Jumapili ya Pasaka wa kike ni 28 na
kiume 26.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Muuguzi
Mkuu wa zamu,Yohana Sehaba alisema kuwa watoto hao ambao walizaliwa
baada ya mama zao kufikishwa hospitalini hapo wakati wa mkesha wa Ijumaa
Kuu na wa Pasaka, hali zao zinaendelea vizuri.
“ Watoto wote waliozaliwa wakati wa Ijumaa Kuu hadi leo jumatatu
tunavyo sherehekea Pasaka wote wazima na afya zao njema baadhi yao
wameruhusiwa na wengine bado wanaendelea na matibabu madogo,” alisema
Sehaba.
Alisema kati ya watoto hao tisa walizaliwa kwa njia ya upasuaji na hali za mama zao hali zao zinaendelea vizuri.
Kwa upande wake, Muuguzi Mkunga wa zamu, Happy Matovu, alisema
hakuna matatizo yoyote waliyopata watoto hao wakati mama zao
wakijifungua.

Comments
Post a Comment