MADONNA KUKUTANA NA RAIS WA MALAWI
Madonna ameasili watoto kutoka Malawi
Msanii wa kimataifa
Mmarekani, Madonna anafanya mkutano na rais wa Malawi, Joyce Banda
kujaribu kusuluhisha mzozo kuhusu kazi ya misaada ya msanii huyo nchini
humo.
Mwezi Disemba,shirika la misaada linalomilikiwa na Madonna lilitangaza kuwa limejenga shule kumi nchini Malawi.Hata hivyo waziri wa elimu Eunice Kazembe, alisema kuwa Madonna ameweza tu kujenga madarasa kumi katika shule zilizopo.
Madonna ameasili watoto wawili, kutoka Malawi, na aliahidi kuwarejesha nyumbani kwao baada ya miaka michache

Comments
Post a Comment