MUME WA LADY JAY DEE GADNER G HABASH AFUNGUKA JUU YA TWEET ZA LADY JAY DEE SOMA HAPA.




gadner_habash


Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayejulikana kama Queen wa bongo Fleva Judith Wambura ‘Lady JayDee’ kuonekana kutuma ‘Tweets’ zilizobeba mafumbo  huku akitoa mazito ya moyoni juu ya mtu anayemvurugia mipango yake ya kimuziki hakuweza kumtaja jina  mume wake Gadna Habash afunguka juu ya ‘Tweets’ hizo

Akizungumza jijini Dar es Salaam hili hivi karibuni Gadna alisema kuwa ‘tweets’ alizoziweka msanii huyo zinalenga kufikisha ujumbe alioukusudia hususani kwa baadhi ya watu wanaomuwekea mipango mibaya ya kuharibu kazi zake za kimuziki

Alisema kuwa wapo baadhi ya washika dau wanaojikita katika maswala ya muziki kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wakimnyonya mwanamuziki bila ya kujali jasho lake na nguvu yake kwa kazi anayoifanya

Kutokana na hali ya kunyonywa wasanii na washika dau hao alisema msanii atakapopata akili na kuwa na uwezo wa kugundua kuwa ananyonya na hawezi kufika mbali hali inabadilika kwa kuanza kukandamizwa na kuwekewa vikwazo katika kazi zao

“Baadhi ya washika dau wanawaogopa wasanii wakubwa kwa kuwa tishio katika biashara zao hivyo hata wasanii wachanga pia wananyimwa nafasi ya kukua kisanii kwa kuhofia kuja kuwageuka baadaye pindi watakapopata nafasi ya kufanya hilo” alisema Gadna

Aliongezea kuwa mfumo wa muziki hauko sawa na upo kwa lengo la kumnyonya msanii hali ambayo inazidi kudidimiza wasanii na muziki wa nchi hii hali inayosababisha muziki unakuwa kwa kusikilizwa redioni na si kwa kukuwa kwa kipato kwa wasanii

Alisema kuna hujuma zinazoendelea kwenye soko la muziki zenye lengo la kumnyonya mwanamuziki na kumpa utajili mdau wa muziki sababu hiyo inapelekeea wanamuziki wa nchi yetu kutoendelea katika soko la muziki

Lady JayDee hivi karibuni amekuwa akitumia mtandao wa Twitter kwa ajili ya kutuma  ’tweets’ zenye ujumbe kwa mtu aliyemkusudia ingawa hazikuonyesha wazi wala kutaja jina la muhusaka

Hizi ni baadhi ya ‘tweets’ zilizotumwa na msanii huyo
Lady JayDee ?@JideJaydee
Hata nyimbo zisipopigwa now mi sio underground, won’t complain. Nani asiemjua JayDEe? Am not crazy

Lady JayDee ?@JideJaydee
Basi mjue kuwa tatizo langu sio nyimbo kutopigwa redioni. Its more than that. U dig??

Lady JayDee ?@JideJaydee
Now nategemea nguvu ya uma #diehardfans

Lady JayDee ?@JideJaydee
Na tweet hivi sbb sikuwahi kulalamika nikaamua kufanya kazi. Lakini kazi inapowekewa uzito wa jiwe isipenye. That’s another case (22)

Comments