Skip to main content
MWAKYEMBE MGENI RASMI MEDIA DAY BONANZA
WAZIRI wa Uchukuzi Dk.
Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo
vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA). Bonanza
hilo litafanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar
es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Pamoja
na mambo mengine, Waziri Mwakyembe atakabidhi zawadi za vikombe na
medali kwa washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa
ya kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo. Lengo
la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni
wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana
mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka,
likiandaliwa na TASWA. Bonanza
hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari
litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote
vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki. Tunataka
bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia mgeni rasmi, burudani,
michezo na mambo mengine yawe ya kuvutia, ambapo Alhamisi Aprili 4,2013
saa tano asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City
Sports Lounge, Posta Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi
yatakayotumbuiza kwenye Media Day na tunatarajia makundi hayo nayo
yatakuwepo kwenye mkutano huo. Tunaomba
vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya
maandishi vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko,
vinginevyo ushiriki wao hautathaminika. Bonanza
litaanza saa tatu asubuhi, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa
ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100,
kuruka kichura, kuvuta
Comments
Post a Comment