Rais Kikwete Azungumza na Naibu Rais Mteule wa Kenya, Ruto
Rais
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule
wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya
kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara.
Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais pia alimueleza Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo. Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.

Comments
Post a Comment