RIPOTI KUHUSU WATOTO WA NELSON MANDELA KUGOMBANIA MALI
BBC wameandika kwamba watoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson MandelaMakaziwe na Zenani Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki wakidai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambae aliondoka hospitali baada ya kutibiwa mapafu akiwa tayari kalazwa hospitali mara nne katika kipindi cha miaka miwili.
Kumekuwa na mzozo wa chinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususani picha alizokuwa anachora akiwa jela ambapo Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa Bizo ambae ni Waziri wa nyumba, Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings kulingana na gazeti la Star.
Bizos akiwa ni wakili anayeheshimika sana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa Mzee Mandela amesema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo na kwamba Watoto wa Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa.
Comments
Post a Comment