Mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa), amefanyiwa
unyama wa kutisha na baba yake wa kambo kwa kunajisiwa, kulawitiwa na
kulazimishwa kulamba mbegu zake za kiume.
Mtoto huyo anayeishi
mkoani Pwani, imedaiwa ana hali mbaya kiafya kutokana na kudaiwa
kufanyiwa kitendo hicho kwa muda wa miaka miwili.
Mwanaume anayedaiwa kufanya unyama huo amefahamika kwa jina la Adam Taliani maarufu kama `Kiredio' (37). Inadaiwa
kuwa baba huyo alikuwa akifanya kitendo hicho mbele ya mama wa mtoto
huyo ambaye ni mke wake, akiwatishia kuwaua kwa panga kama watatoa siri
hiyo.
Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa mtoto huyo Chiku
Selemani alisema vitendo hivyo alianza kufanyiwa na baba yake wa kambo
tangu mwaka 2011 wakati mama yake alipoanza kuishi na mwanaume huyo.
Alisema,
waligundua unyama huo baada ya mtoto huyo kuanza kusema kwa majirani
zao jinsi baba yake anavyomfanyia vitendo hivyo usiku huku mama yake
akishuhudia.
"Hapo mwanzo tulikuwa tunasikia kwa majirani kuwa
mtoto wetu anasimulia mambo mazito, hata hivyo hatukumuamini sana,"
alisema Chiku.
Chiku alisema kitu ambacho kinamsikitisha kuona
dada yake ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa akishuhudia
jambo hilo na wakati mwingine walikuwa wakiingiliwa kwa zamu yeye na
mtoto wake.
GIZA LA UNYAMA
Akisimulia huku akimwaga
machozi, mtoto huyo mbele ya mwandishi wa blogu hii kuwa baba yake alianza
kumuingilia wakati walipohamia kijiji cha Soga, Wilaya ya Kibaha mwaka
2011.
Alisema siku moja usiku wakati amelala, alimuona baba yake
akimshika na kumlazimisha kumuingilia huku akimtisha kumkata kwa panga
endapo atapiga kelele.
Alisema, aliogopa sana, alimuacha baba yake afanye anavyotaka na hapo ndipo ukawa mlolongo wa kufanyiwa unyama huo kila siku.
"Anaponiingilia napata maumivu makali, nataka kupiga kelele lakini naogopa ataniua kwa panga," alisema mtoto huyo.
Mtoto
huyo alizidi kusema kwamba kwa kuhofia kuendelea kufanyiwa vitendo
hivyo, aliamua kutoroka nyumbani kwao kila siku nyakati za jioni na
kwenda kwa majirani, lakini wazazi wake walimtafuta na kumrudisha
nyumbani.
Kutokana na kutoroka mara kwa mara, uongozi wa kijiji
hicho uliamua kuwafukuza kijijini hapo na walirudi Mwandege mwishoni mwa
mwaka huo.
"Tuliporudi baba alizidi kuniingilia, sasa ilikuwa
anafanya kwa zamu, akitoka kwa mama anakuja kwangu na kuniingilia sehemu
zote za siri," aliongeza kusema.
MAMA ASAIDIA KUEPUSHA KUNYIMWA UGALI
Hata
hivyo alisema wakati anafanyiwa matukio hayo, mama yake anakuwa
akishuhudia, wakati mwingine anamsihi asikatae anapoingiliwa kwa sababu
watakosa chakula.
"Kila kitu ninachofanyiwa mama anakiona,
nipapokataa mama ananiambia nisifanye hivyo ili tuendelee kula ugali wa
baba," alisema mtoto huyo.
Alisema kutokana na kufanyiwa vitendo hivyo anaona sehemu zake za siri zimeharibika kwa vidonda.
ALAZIMISHWA KULA MBEGU ZA KIUME
Katika
jambo la kusikitisha zaidi, mtoto huyo kabla na baada ya kuingiliwa
hulazimishwa kula mbegu za kiume za baba yake ili kumsafisha.
Alisema,
wakati baba yake anapomaliza kufanya mapenzi na mama yake, humfuata na
kumwambia alambe mbegu zote, kisha anamuingilia mtoto huyo na
anapomaliza humlazimisha tena kumsafisha kwa kumlamba.
NDUGU WAINGILIA KATI
Mama
mdogo wa mtoto huyo, Chiku alisema baada ya kupata taarifa hizo,
walilifikisha suala hilo ngazi ya ofisi ya kitongoji, kijiji na kituo
cha polisi kwa ajili ya kumsaidia.
Alisema kwa kushirikiana na
polisi wa kituo hicho, alifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya
Temeke, ambapo huko ilibainika mtoto huyo ameathirika na magonjwa ya
zinaa.
Chiku alisema kwenye vipimo hivyo, iligundulika tumbo lake limejaa uchafu na alipatiwa huduma ya kumuondoa uchafu.
"Walinishauri
kutokana na afya ya mtoto kuwa mbaya, nimpeleke hospitali ya karibu ya
Mkuranga, huko atapewa huduma zote kulingana na magonjwa aliyokuwa
nayo," alisema.
Alisema kutokana na kuwa peke yake katika suala
hilo, hakuweza kuendelea nalo na badala yake aliliacha na kuendelea
kuishi na mtoto huyo katika hali ngumu.
Chiku alisema hawezi
kumlaumu sana dada yake, kwa sababu ana matatizo ya akili, ndio maana
mwanaume huyo anaweza kufanikisha mambo yake bila kizuizi.
Alisema
kutokana na maisha magumu anayoishi, hawezi kushughulikia tatizo hilo
na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua, aliomba watu binafsi mashirika
mbalimbali ya haki za binadamu kuingilia kati.
Pamoja na hayo,
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Urich Matei, alipoulizwa suala hilo,
alisema bado hajalipata, akamuomba mwandishi asubiri ufafanuzi baada ya
kupata taarifa kutoka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga.
"Taarifa
hiyo sijaipata, ni mpya kwangu nakuomba niwaulize wenzangu wa Mkuranga
na baadae nitakupatia ufafanuzi," alisema Kamanda Matei.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwandege Ally Ubuguyu alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alithibitisha kutokea.
Ubuguyu
alisema baada kupata taarifa hizo, wametoa taarifa katika kituo cha
Polisi Vikindu, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
"Mtuhumiwa bado yupo hapa kijijini, lakini hakuna polisi aliyekuja kumkamata pamoja na kutaarifu juu ya tukio hili," alisema.
Alisema
uongozi wake upo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa Polisi
watakaokwenda kumkamata mtuhumiwa huyo, kwani kitendo alichokifanya ni
kibaya. |
Comments
Post a Comment