SOMA HAPA KUHUSIANA NA UJUMBE WA MAGAIDI KUTOKA SOMALIA POLISI KUKESHA MACHO MJI KASORO BAHARI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.
.
Kwa mujibu wa ujumbe huo uliosambaa unasomeka: “Tahadhari kundi la kigaidi kutoka Somalia tayari limekwisha wasili mkoani Morogoro kwa ajili ya kubomoa na kuchoma makanisa wakati wa sherehe za Pasaka, tunatakiwa kuwa makini tuwapo makanisani na hata katika kazi zetu, usipuuze, wajulishe wachungaji, wainjilisti na wakristo wote ni vema na haki kusambaza ujumbe huu”.
Ujumbe huo ambao umezagaa kila kona ya mkoa wa Morogoro na mikoa mingine, umedumu kwa wiki moja sasa na kusababisha hofu kwa waumini waliotarajia kwenda makanisani katika sikukukuu hizo.
Kusambaa kwa ujumbe huo kulilifanya Jeshi la Polisi mkoani hapa kuweka ulinzi mkali katika makanisa mbalimbali ya Morogoro hususan wakati wa mkesha wa Pasaka, ambapo baadhi ya watu walionekana kuzungukazunguka makanisa hayo na haikujulikana haraka kama watu hao walikuwa ni askari polisi au ni kikundi maalum cha ulinzi cha makanisa hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alithibitisha kusambazwa kwa ujumbe huo wa vitisho katika mitandao wa kuwepo kwa kikundi cha El-shabaab kutoka Somali na kusema kwamba hazikusambazwa Morogoro pekee bali karibu nchi nzima.
Alisema hata hivyo uvumi huo haukuleta athari zozote kwa wananchi na kwamba sikukuu ya Pasaka kwa mkoa wa Morogoro imekwenda vizuri na hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa za kuweko kwa matukio ya kihalifu.
Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki Mkoa wa Morogoro, Askofu Telesphone Mkude, akitoa mahubiri yake katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick, alisema ujumbe huo unaosambazwa hauna lengo jema kwa waumini wa dini hiyo kwani unataka kuwatisha waumini ili wasiende makanisani kwa ajili ya kuabudu

Comments
Post a Comment