SOMA HAPA SHEIK PONDA ATAPONA KWELI KESHO

2nd April 2013
Sheikh Issa Ponda
Mawakili wa Jamhuri na wale wa utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49, kesho  wanatarajia kuwasilisha kwa njia ya maandishi hoja za kama washtakiwa wana hatia au la, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake baada ya washtakiwa wote kujitetea mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa anayesikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Juma Nassoro alidai kuwa amefunga ushahidi dhidi ya Jamhuri baada ya washtakiwa wote kutoa utetezi wao mahakamani hapo.

Awali upande wa Jamhuri uliita mashahidi 17 kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Hakimu Nongwa alisema mawakili wa pande zote mbili watawasilisha hoja zao kwa njia ya maandishi Aprili 3, mwaka huu za kama washtakiwa wana hatia au la.

Mbali ya Ponda washtakiwa wengine ni, Sheikh Mukadam Saleh, Kuluthumu Mohamed, Zaldah Yusuph, Juma Mpanga, Farida Lukoko, Adamu Makilika, Athum Salim, Seleman Wajumbe, Salum Juma, Salum Mkwasu na Ramha Hamza.

Wengine ni, Halima Abas, Maua Mdumila, Fatihiya Habibu, Hussein Ally, Shaban Ramadhani, Hamis Mohamed, Rashid Ramadhani, Yusuph Penza, Alawi Alawi, Ramadhani Mlali, Omary Ismaili, Salma Abduratifu, Khalidi Abdallah, Said Rashid, Feswali Bakari, Issa Wahabu, Ally Mohamed, Mohamed Ramadhani, Abdallah Senza, Juma Hassani na Mwanaomary Makuka.

Wengine ni, Omary Bakari, Hamza Ramadhani, Ayubu Juma,Maulid Namdeka, Farahan Jamal, Smalehes Mdulidi, Jumanne Mussa, Salum Mohamed, Hamis Halidi, Dite Bilali, Amiri Said, Juma Yassin, Athuman Rashid, Rukia Yusuph, Abubakari Juma na Ally Salehe.

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa  katika shtaka la kwanza, Oktoba 12, mwaka 2012  huko Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 50 walikula njama ya kutenda makosa.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku ya tukio la kwanza, eneo la Chang’ombe Markas, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 50 kwa jinai walivamia   kwa nia ya kutaka kujimilikisha kiwanja mali ya Agritanza Ltd.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la tatu kuwa, kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka 2012, Chang’ombe Markas pasipo uhalali na hali ya uvunjifu wa amani washtakiwa wote kwa pamoja walijimilikisha ardhi ambayo ni mali ya Agritanza Ltd.

Shtaka la nne, ilidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka 2012, Chang’ombe Markas washtakiwa wote kwa pamoja waliiba vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo matofali 1,500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh. 59,650,000 mali ya Agritanza Ltd.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa katika shtaka la tano linamkabili Sheikh Ponda peke yake, kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka 2012, Chang’ombe Markas, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania, aliwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya jinai.

Washtakiwa wote walikana mashtaka yao kwa nyakati tofauti.

Mapema Oktoba 18, mwaka 2012, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka yao, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), aliwasilisha hati ya kiapo cha kupinga dhamana ya Sheik Ponda na Mukadam kwa usalama wake na maslahi ya taifa

Comments

Popular Posts