WATU
zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba
mchanga aina ya Moramu katika machimbo yaliyopo Moshono nje kidogo ya
jiji la Arusha.
Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio
kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi
wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .
Pamoja
na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya
baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50
kutoka usawa wa bahari.
Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni Jeshi la
Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya
marehemu 16 waliofukiwa.
Baadhi ya miili ya marehemu imetambulika
kwa majina kuwa ni Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu),
Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na
Garald Masai.
Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha
kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini
Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya
mvua. |
Comments
Post a Comment