WATU 17 WAHOFIWA KUFA NA MIILI 13 YA WATU YAOPOLEWA MARA BAADA YA KUANGUKA KWA KIFUSI HUKO ARUSHA

                                    

                             

 MOJA YA MWILI WA MAREHEMU  ULIOTOLEWA KWENYE KIFUSI

 Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.

habari  za kuaminika kutoka katika chanzo kimoja jijini Arusha wapakiaji  17 wanahofiwa kufariki dunia na tayari miili ya marehemu 15  imeshatolewa kutoka katika kifusi cha kokoto(moramu) huko Arusha.

akiongea na jamiileotz.blogspot.com kwa njia ya simu shuhuda wa tukio hilo kutoka Arusha anasema tukio hilo limetokea leo majira kati ya saa 4 na saa 5 asubuhi mara baada ya kuanguka kwa kifusi cha kokoto wakati wapaikiaji hao wakiwa shimoni wakipakia kokoto.


ajali hiyo ya kuanguka kwa kifusi imehusisha magari mawili kufukiwa na kokoto ambapo ni lori  lilojulikana kama chombo cha neena pamoja na lori aina ya scania amabyo mpaka sasa bado yamefukiwa na kokoto pia yameharibika vibaya hivyo namba zako kushinda kutambulika mara moja.

 uokozi bado unaendelea ili kutoa miili ya wale waliokutwa na  tukio hili na pia jitihada zinafanyika kama kutaopolewa wengine wakiwa hai.

mlima wa moram uko nje kidogo ya jiji la Arusha katika eno la pekas kama unaelekea nduruma  mbele kidogo ya mji wa  Moshono


Mungu ametoa na Mungu  ametwaa jina lake lihimidiewa Jamiileotz.blogspot.com linatoa pole sana kwa wahanga wa tukio hili

Comments

Popular Posts