DIVA WA CLOUDS FM AMPA SUPPORT "MKE MWENZA WA KENYA " ANAYEIWAKILISHA NCHI HIYO KWENYE BIG BROTHER AFRICA
Huddah Monroe a.k.a The boss lady ambaye ni model mwaka huu ndio amebeba imani za wakenya za kurudi na kitita cha $300,000 zinazoshindaniwa katika msimu wa 8 wa shindano la Big Brother “The Chase” baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ya jirani.
Siku chache zilizopita jina la Huddah limeonekana kupata umaarufu zaidi Tanzania hasa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya binti huyo mwenye historia ya matukio mengi ya utata huko Kenya (pamoja na kujihusisha na upigaji wa picha za utupu) kujikuta anaingia katika ugomvi wa maneno na mtangazaji maarufu hapa Tanzania Loveness Love a.k.a Diva kutokana na kinachoaminika kuwa sababu ni Prezzo.
Diva a.k.a mimi Kupitia akaunti yake ya twitter, juzi (May 26) aliandika tweet inayoonesha kuweka kando tofauti alizokuwa nazo na Huddah na kuahidi kumsupport kwa kutokumwandikia “shit” kama njia ya kumuunga mkono “wifi” katika BBA.
Diva amekuwa akidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper kutoka Kenya CMB Prezzo, kitendo kilichopokelewa tofauti na mrembo Huddah ambaye pia kulikuwa na tetesi aliwahi kudate na “Liq Her” hit maker, Rapcellency, Prezzo
wasiliana nami kupitia faceboook.com na twitter.com halafu unaweka slashi abdalla wellah.
wasiliana nami kupitia faceboook.com na twitter.com halafu unaweka slashi abdalla wellah.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment