KAMA ULIMISI KUSIKILIZA KESI YA KUSAFIRISHA WANYAMA HAI .SOMA HAPA
8th May 2013
B-pepe
Chapa
Mashahisi zaidi ya 50 wanatarajia kutoa ushahidi wao na vielelezo vilivyopo takribani 100 vitatumika.
Akiwasilisha taarifa ya kukamilika kwa upelelezi huo na kukamilika kwa mashahidi na vielelezo hivyo mbele ya Hakimu Mkazi, Simon Kobelo, Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri, Eveta Mushi, alidai kuwa mashahidi wapo zaidi ya 50, lakini hawawezi kutajwa hadharani.
Kufuatia hali hiyo, mawakili wa upande wa washitakiwa waliomba kutajwa kwa vielelezo hivyo, lakini Mushi alikataa na kudai kuwa siyo takwa la kisheria kutaja majina ya mashahidi na vielelezo kabla kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Kufuatia hali hiyo, upande wa utetezi ulidai kuwa lengo la Jamhuri ni kuchelewesha kesi hiyo na kuiomba mahakama kutaja japo baadhi ya vielelezo jambo lililopingwa na Mushi.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kusafirisha wanyama hai 136 na ndege hai kwenda Doha, Qatar kwa kutumia ndege aina ya C.17 yenye nambari AMA/MAB, mali ya Shirika la Ndege la Qatar na kuwapitisha kwenye geti namba 5A na 5B katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).
Washitakiwa hao ni Kamran Mohamed ambaye ni raia wa Pakistani, Hawa Hassan, Martin Methew na Michael Disha na wote walikana shitaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 11 na 12 itakapoanza kusikilizwa na mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao.
CHANZO: NIPASHE

Comments
Post a Comment