SOMA KAULI YA WAZIRI MEMBE KUHUSU UJIO WA OBAMA TANZANIA
24th May 2013
B-pepe
Chapa
Membe alizungumza hayo jana katika wa mkutano baina yake na mabalozi wa nchi za Umoja wa Afrika nchini pamoja na wanahabari jijini Dar es Salaam.
Membe alisema fedha hizo zitasaidia kukamirisha miradi mbalimbali katika sekta za barabara, maji na elimu, akiwa nchini rais Obama ataongozana na ujumbe wa wafanyabiashara 700.
Kwa mujibu wa Membe, rais Obama atafanya mkutano na wakurugenzi wa mashirika makubwa kwa pamoja na wale kutoka Marekani huku ujumbe wa mkutano huo ukiwa Power Afrika (Saidia Afrika).
Pia rais Oboma ambaye katika ziara yake ataambatana na mkewe Michele Obama, atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Kikwete.
Alisema kabla ya kuwasili kwake nchini, tayari ameshatuma timu kwa ajili ya kumwandalia mazingira ya ujio wake huo huku ya pili ikitarajiwa kuwasili muda wowote.
Membe aliongeza kuwa, ujio wa Obama Julai Mosi na 02, mwaka huu utakutana na mambo mengi muhimu yakiwamo ya ‘smart dialogue partnership’ yatakayofanyika nchini kwa kujumuisha nchi mbalimbali huru za Afrika.
Aidha, aliwataka wafanyabiashara mbalimbali wakiwamo wa vyombo vya usafiri kama vile teksi na wamiliki wa hoteli kutumia vizuri fursa hiyo ya takribani wiki nzima kwa kuanza na ugeni wa smart dialogue partinership ambao wataanza kuingia mwishoni mwa mwezi huu.
Kuhusu maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kwa Umoja wa Afrika (AU) wakati huo Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule alisema yatafanyika Mei 26, mwaka huu katika nchi zote za Afrika huku kibara yakifanyika katika makao makuu ya Umoja huo, mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Kwa mujibu wa Haule, hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Karimjee huku mgeni rasmi akiwa Waziri Membe.
Alisema kwa Tanzania kufanya maadhimisho hayo ni muhimu kwani ilihusika kwa sehemu kubwa kuzisaidia nchi za Afrika kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni.
Aliyataja mafanikio ya umoja huo wakati huo ni nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kutoka 32 hadi 53 tangu kuanzishwa kwake Mei 1963 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Comments
Post a Comment