Mwanafunza wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma aliyekuwa akisoma mwaka wa pili (Diploma in Business Administration) Bw. Frank ndakidemi jana Tarehe 09/06/2013 siku ya Jumapili alifariki Dunia kwa ajali ya pikipiki wakati akitokea maeneo ya Area D (barabara ya njia panda Area D). Hata vivyo ajali hiyo ilitokea Asubuhi sana mnamo saa 12 ,wakati Marehemu alipokuwa akiendesha pikipiki na kisha kugongana na gari aina ya Hiace. Hata hivyo ajali hiyo ilimpelekea kuumia vibaya maeneo mbalimbali ya mwili hatua iloyosababisha apoteze maisha,kufuatia ajali hiyo jeshi la Polisi limeendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Aidha mwili wake ulihifadhiwa katika Hospital kuu ya mkoa wa Dodoma ili kusubiri taratibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua ya kusafirisha Mwili huo. Katika hatua nyingine Marehemu alipata ajali akiwa amempakia rafiki yake(jina lake halikupatikana mara moja) ambaye kwa upande wake aliumia na amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma Wodi namba kumi,ambapo anaendelea na matibabu. Akizungumza na chanzo chetu cha Habari Mshauri wa wanafunzi wa CBE Bw. Sikato amesema "Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa leo chuoni hapo ikiwa ni baada ya mzazi wa(Baba) kuwasili jana usiku akitokea Iringa ,kisha Mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Moshi ambapo hatua mbalimbali ikiwemo mazishi zitafanyika" Kwa hakika Musiba huu uliibua simanzi sana kwa wanafunzi wote wa CBE. Akizungumza na chanzo chetu cha habari Bw.Remidius Emmanuel (Aliyekua kiongozi wa COBESO) Amewataka wanafunzi wote wa CBE kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na kuzidi kumuomba MUNGU ili kuwa wastahimilivu wa matukio kama haya, Hakika hii ni safari ya kila mmoja wetu ila mwenzetu katangulia, Alisema Bw. Remidius" |
Comments
Post a Comment