MKE WA KANYE WEST KIM KARDASHIAN AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE HABARI KAMILI SOMA HAPA



NI siku ya furaha kwa Kanye West! Kim Kardashian amejifungua mtoto wa kike Jumamosi asubuhi katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center, Los Angeles, mtandao wa OMG umethibitisha.

Inasemekana Kardashian, 32, alikuwa na West pembeni mwake wakati wa kujifungua, kumkaribisha duniani binti yao mwezi mmoja kabla ya muda uliotarajiwa. Tarehe halisi ya kujifungua ilitazamiwa kuwa Julai 11.

"Kim aliugua Ijumaa usiku na hatimaye kupata mtoto mapema jumamosi," chanzo cha hospitali kimeileza Us Weekly. “Inafurahisha, wote wako katika hali nzuri!"

Kanye West, 36, na Kim - wote wawili wakiwa ndo mara ya kwanza kuwa wazazi, wamekuwa wapenzi tangu Aprili 2012.

Desemba 30, 2012, West alitangaza kwamba mpenzi wake alikuwa na mimba wakati wa tamasha lake Atlantic City.

"Simamisha muziki na wote mpige kelele kwa mama kijacho," alisema West jukwaani akionyesha kidole kwa Kim ambaye alikuwa mmoja wa  watazamaji.

Comments