CHEKI PICHA ZA RAIS OBAMA NA FAMILIA YAKE WALIPOTEMBELEA KISIWA CHA GEREZA LA "ROBBEN" ALIPOKUWA AMEFUNGWA "NELSON MANDELA" WAKATI WA KUPINGA UBAGUZI WA RANGI

Rais wa Marekani Barack Obama akitazama chumba namba 5. katika gereza la Robben ambamo katika chumba hiki ndimo Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alipofungiwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyofungwa jela. 

Rais wa Marekani Barack Obama pamoja na familia yake wametembelea kisiwa cha Robben nchini Afrika ya Kusini ambako ndipo Nelson Mandela nawenzake waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi waliko fungiwa kwa miaka 18.
Rais wa Marekani Barack Obama akitazama chumba namba 5. katika gereza la Robben ambamo katika chumba hiki ndimo Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alipofungiwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyofungwa jela.
Rais Obama akiwa na mke wake Michelle Obama siku ya Jumapili ya tarehe 30 wakati walipotembelea Gereza la Robben lililoko kisiwani ambako Mandela na wenzake wapigania haki za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini walikofungwa hapa.
Rais Obama na familia yake pia walitembelea "rock quarry" sehemu ambako Nelson Mandela na wafungwa wenzake walipokuwa wakilazimishwa kufanya kazi katika eneo hilo lililoko ndani ya kisiwa cha Robben.
Kutoka kushoto ni Michelle Obama, Sasha Obama, Ahmed Kathrada mfungwa aliyekuwa pamoja na Nelson Mandela Gerezani kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyofungwa Mandela, Rais Barack Obama, Marian Robnison na Leslie Robinson. 

Comments