KAMA ULIMISI HABARI YA JAMBAZI SUGU KUUAWA MKOANI ARUSHA,TUKIO ZIMA LILIKUWA HIVI SOMA HAPA
Jambazi
Sugu afariki katika majibishano ya
silaha na polisi katika tukio tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi
la polisi baada ya kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini
hapa jana majira ya jioni.
Kwa mujibu
wa kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas
alisema kuwa mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa Onjaftian jeshi hilo
lilifanikiwa kumuuwa baada ya majibishano ya risasi na askari wa jeshi hilo
jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris Taiko au kwa majina mengine
doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri wa miaka32-35 mkazi wa sokon 1
jijini hapa.
Kamanda
alisema kuwa awali walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3
wanaosadikiwa majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira nyumba
walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha ghafla risasi
zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari hali iliyowalazimu
askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi huyo.
Sabas
alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa ni
jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki kwenye matukio
ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam na
alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta iliyofutwa namba risasi moja
chemba,ganda moja la risasi iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya
shortgun,na funguo mbali mbali 26 na mordem ya kampuni ya Airtel.
“Jambazi
huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki kwenye
matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo
lilitokea28\08\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora bastola
yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.
Katika tukio
lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini jeshi la
polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la peter Toshi katika
majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina tisas inayoaminiwa kuwa ndio
ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.
Kamanda
sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio anabainisha kuwa mmiliki wa nyumba
aliokuwa jambazi huyo anaefahamika kwa jina moja la Swalehe au baba Amiri
ambaye hakuwepo wakati wa tukio hili jitihada za kumtafuta zinafanyika ili
aweza kuhojiwa juu ya uhusiano wao na jambazi aliyeuwa na wapangaji wengine kwenye
nyumba hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.
Hata hivyo
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka
majmbazi wengine badao zinaendelea kufanyika.
Comments
Post a Comment