KAMA ULIMISI KUSIKIA WATANZANIA 60 KUKAMATWA AFRIKA KUSINI WAKATI WA ZIARA YA OBAMA SOMA HAPA HABARI KAMILI
Watanzania 60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.
Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri hatua za kisheria zaidi.
Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini juzi na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.
“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.
Leo mchana Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.
Comments
Post a Comment