KUWA WAKWANZA KUSOMA HABARI HII YA HAWA WAMASAI WALIOMBAKA MKE WA MWENZAO

 
Wamasai wawili wamekamatwa na polisi kufuatia tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15 eneo la Goba, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Elisoloi Leid (17) na Jackson James (12), wote wakazi wa Goba jijini Dar es Salaam ambao wanatuhumiwa kumbaka mke wa mmasai mwenzao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Wamasai hao walifanya kitendo hicho Jumatano wiki hii majira ya asubuhi, muda mfupi baada ya mwenye mke kuondoka kwenda kwenye shughuli zake.
Mmoja wa mashuhuda hao, John Isack alisema kuwa, wamasai hao walikutwa wakimbaka binti huyo wakati mafundi ujenzi walipofika asubuhi kuchukua vifaa vya ujenzi kwenye nyumba wanayoishi.
Alisema kuwa mafundi hao walikuta mlango wa nyumba umefungwa na walipogonga bila kufunguliwa walisikia sauti ya msichana ndani ikilia. Ndipo mmoja wa mafundi hao alipopiga teke mlango na kuwakuta wamasai hao wakimbaka binti huyo.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi eneo hilo walijitokeza na kuwazingira kwa kuwaweka chini ya ulinzi, huku wengine wakiwa wameshika silaha mbalimbali za jadi kuwatishia wasikimbie mpaka hapo polisi watakapokuja kuwachukua.
Wamasai hao walishikiliwa na wananchi hao kwa muda wa nusu saa na baadaye pikipiki mbili zilikodiwa ambapo moja ilimbeba binti huyo na nyingine watuhumiwa na kupelekwa kituo cha polisi cha Kawe kwa hatua zaidi.
Shuhuda mwingine Amina Mohamed, alisema kuwa unyama aliofanyiwa binti huyo umetokea siku chache baada ya kuja jijini Dar es Salaam kuishi na mume wake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mume wa binti huyo kwa jina moja la Saaya.
Kamanda Wambura alisema Saaya aliwaleta watuhumiwa hao kutoka umasaini kwa lengo la kuwatafutia kazi za ulinzi. Alisema siku ya tukio, aliondoka asubuhi na kuwaacha wakiwa na mke wake, ndipo walipombaka. Kamanda alisema Saaya na mke wake waliondoka siku ya pili yake baada ya kutoa maelezo polisi kuelekea kijijini kwao.
Wambura alisema wanaendelea kuwashikilia wamasai hao kwa uchunguzi zaidi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani

Comments