,RAIS KIKWETE LEO KUCHEZESHA MECHI YA WABUNGE WA YANGA NA SIMBA UWANJA WA TAIFA LEO KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI soma hapa kwa taarifi zaidi

.
Naona hii ni historia kabisa aisee….. yani Rais Jakaya Kikwete anaweza hata kuingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia kwa kukubali mwaliko wa kuwa refa na kuchezesha mechi ya Wabunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa timu za Simba na Yanga jumapili July 7 2013.
Taarifa ambayo nimepewa na Global Publishers ambao ndio waandaaji, ni kwamba Rais amekubali kuwa refa kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya mapato yake yatasaidia elimu Tanzania.
Ni mara ngapi tunamuona President wetu kwenye sehemu rasmirasmi akiwa mgeni rasmi? ni mara ngapi tunatamani kuona upande wake wa pili kwenye ishu kama hizi? basi Jumapili hii itakua burudani na pia vichekesho… yani ukijaribu kutengeneza picha President na umri wake, na umbo lake, na cheo chake alafu apulize filimbi?????
Yani anakuwa refa na jezi zake kabisa…. na tumeshamzoea siku zote huwa anatokelezea hivi yani….
.
.
.Jakaya Kikwete 4
.

Comments