SHILOLE ANASWA AKIINGIA SUPERMARKERT NA TAULO LA KUOGEA PICHA YA TUKIO IKO HAPA

 MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoa kali ya mwaka baada ya kunaswa akiingia ‘supermarket’ akiwa ametinga taulo

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika mji wa Maryland nchini Marekani ambapo staa huyo amekwenda kwa ajili ya kufanya shoo kisha kupigwa picha hiyo na rafiki yake ambaye aliiweka mtandaoni ikimuonesha akiwa amefunga taulo kwenye matiti.
Mwandishi wetu alipomuuliza Shilole kutokana na kitendo alichokifanya kupitia mtandao wa Instagram, alifunguka:
“Huku watu wanaishi kizungu hakuna mtu anayeshughulika na maisha ya mwenzake kila mmoja anahangaika na mambo yake kwa hiyo siyo ajabu mimi kuvaa taulo na kwenda nalo supermarket, huku ni kawaida tu.”

Comments