WABUNGE MASHABIKI WA YANGA WATWAA KOMBE BAADA YA KUWAFUNGA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA MBELE YA REFA RAIS KIKWETE
baada ya kuanzisha mpira akimpa refa filimbi aendelee |
Kipa
hodari kwa michomo ya penalti wa timu ya wabunge mashabiki wa Simba SC,Ni Mbunge wa Kinondoni, Iddi
Azzan ambaye leo aligeuzwa shati tu langoni baada ya kutunguliwa penalti zote
zilizopigwa na Wabunge mashabiki wa Yanga.
Waliofunga
penalti za Yanga ni Michael Kadebe, Mark Tanda, Christopher Kabenyele
na Said Mtanda, wakati kwa Simba Yona Kilumbi alipaisha ya kwanza, Amos
Makala, Adam Malima na Abel Kigula wakafunga zilizofuata na Aziz Abood
akakosa ya tano.
Kipa wa Yanga, Hussein Zubeiry Mbunge wa Fuoni Zanzibar alisimama imara leo kulinda lango Yanga na kuokoa michomo mingi ya hatari.
Mechi hiyo ilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliyeanzisha kabla ya kumuachia refa Athumani Kazi aendelee kama anavyoonekana hapo chini
Comments
Post a Comment