DAKTARI ALIYEMTIBU SHEIKH PONDA MOROGORO ATIWA MBARONI...... CHAMA CHA MADAKTARI CHAJA JUU .soma habari kamili hapa
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (Moi), jana aliondolewa na kupelekwa katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Kitendo hicho kimelaaniwa vikali na familia yake na wafuasi wake, ambao wamepanga kufanya maandamano makubwa leo ...
Sheikh Ponda, ambaye alisomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu. Alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa.
“Nimepigiwa simu mchana huu na mmoja wa wanafamilia, nimeshangaa sana kwa sababu nakumbuka jana (juzi Jumatano) Sheikh alishindwa kufanyiwa mahojiano na polisi kutokana na kuhisi maumivu na kizunguzungu,” alisema Nassoro.
Comments
Post a Comment