Angalia picha za mbunge wa CCM vicky Kamatta alivyokutwa akichunga mbuzi na soma hapa kauli aliyotoa juu ya tukio hilo
WAKATI ikitarajiwa kwamba angekuwa nyumbani amejipumzisha kutokana na
nafasi yake, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita (CCM), Vicky Paschal
Kamatta, amekutwa akiwa anachunga mbuzi katika moja ya mashamba yake
jijini Dar es Salaam.
Akiwa na kundi la wanyama hao wapatao 27 huku akionekana mwenye dalili za uchovu, mheshimiwa huyo alikutwa maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya jiji ambako aliweka wazi kuwa kuchunga mbuzi ni sehemu ya maisha aliyopitia.
“Alisema alipoulizwa na mwandishi wa blogu hii hili ni shamba langu na hawa ni mbuzi wangu, kazi ya kufuga, siyo Mbuzi tu hata wanyama wengine ni asili yetu kule usukumani, siwezi kuikacha kwa kisingizio cha ubunge,” alisema Vicky ambaye kabla hajawa mbunge, aliwahi kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya.
“Hii ni kazi ambayo nimekua nikiifanya huko nyumbani (Geita), hivyo hata kwa sasa ninapopata nafasi kama hii, hasa mwishoni mwa wiki, huja huku kujikumbushia maisha yangu ya zamani.”
Alisema fikra za wengi kuwa wanasiasa huishi tofauti na wananchi wa kawaida siyo kweli, kwani wengi wao wametoka katika maisha ya kawaida kabisa vijijini.
Kabla hajawa mbunge aliwahi kuwa msanii, alitamba na kibao chake kisemacho Wanawake na Maendeleo na pia alishawahi kuwa mwalimu na alisoma katika chuo cha waalimu cha Mandaka kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.

Comments
Post a Comment