Kamanda Kova awataka Watanzania kufichua wahalifu
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova, amewataka wananchi kuwafichua wahalifu kwa kutoa taarifa kwa siri ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.
Kamanda Kova amewataka wananchi wa Tanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi nchini humo na vile vile amewaasa raia kutojishirikisha katika vitendo vya uhalifu na kuwataka kuwafichua watu wanaofanya makosa ngazi ya familia
. Kamanda Kova amebainisha kuwa, ni ukweli usiopingika kuwa uhalifu mwingi unaanzia ngazi ya familia. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Tanzania amebainisha kwamba, kwa mfano kuna uhalifu wa baba na mama kupigana, ubakaji ndani ya familia, ulawiti, unyanyasaji wa kijinsia na mengine mengi, lakini familia zinayafumbia macho matukio kama haya.

Comments
Post a Comment