Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
November 11, 2013
Waziri mkuu Mizengo Pinda ahidi kupambana na ugaidi uliotokea Mtwara na wilayani Kilindi.
Kwa
Mara
ya kwanza Serikali ya Tanzania imezungumzia madhila iliyofanywa na Jeshi kwa kushirikiana na Polisi wa nchi hiyo japo haikutaja kwa urefu na uapana na kuelezea mauaji hayo ya waislaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali kupitia polisi inaendelea kujipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama, ukiwamo ugaidi/uislaam.
Akitoa hoja ya kuahirisha Bunge Dodoma jana, Pinda alisema matukio ya hivi karibuni nchini
Kenya
na kukamatwa kwa watuhumiwa nchini ni ishara kwamba ugaidi/uislaam hauna mipaka unaweza kutokea nchi yoyote.
Pinda alirejea matukio ya kukamatwa kwa vijana wa kislaam 12 waliokuwa mkoani Mtwara na
wale
waliokamatwa Wilaya ya Kilindi wakiwemo wanawake na watoto,mkoani Tanga, kuwa ni ushahidi unaotoa wajibu wa kuimarishwa kwa ulinzi na kuchukua tahadhari dhidi ya matukio hayo.
“Kila kiongozi wa eneo ajue watu wanaoishi katika himaya yake. Kazi hii itasaidia kuepuka tatizo la wageni wasiojulikana au wahamiaji haramu,” alisema Pinda.
na kuongeza:
“Aidha kamati za Ulinzi na Usalama za mitaa na vijiji zinahimizwa kutekeleza mkakati wa kuzuia uhalifu kwa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi, kwa kuzingatia sheria ya serikali za mitaa na sheria ndogo zilizotungwa ili kuimarisha usalama katika halmashauri husika”.
Alisema Serikali imekuwa ikiwahimiza wafanyabiashara wasaidiane na vikundi vya ulinzi shirikishi huku wale wenye biashara kubwa zenye mikusanyiko ya watu wengi wanaagizwa kufunga
kamera
za usalama na kuziunganisha kwenye mtandao wa polisi ambao wanaweza kutoa msaada pale uhalifu unapotokea.
Chanzo cha Habari: Gazeti la Mwananchi.
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment