Kundi la kigaidi la Al Shabaab yatishia kushambulia Ulaya


Waziri wa Usalama wa Marekani anasema analitia mashaka sana tishio la kundi la Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya maduka huko Marekani, Canada na Uingereza .


Katika mahojiano kwenye televisheni, Jeh Johnson alisema pametokea mabadiliko katika vitisho vya makundi ya wapiganaji Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa washabiki wao katika nchi maalumu kufanya mashambulio.

Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali .

Mwaka wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.

CHANZO : BBC SWAHILI

Comments