Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Labels
event
news
February 22, 2015
Majengo ya kale Bagamoyo hatarini kutoweka
Na : Abdalla Wellah , jamii leo tz
Bagamoyo
Majengo ya Bagamoyo.
Historia ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani iko hatarini kupotea na kupoteza idadi ya watalii wanaotembelea mji huo baada ya vivutio vya kitalii kuachwa vikibomoka bila kufanyiwa ukarabati.
Baadhi ya vivutio hivyo ni makaburi ya kale likiwamo kaburi maarufu la wapendanao ambapo watu huenda kuomba dua wakiamini kupata baraka kwenye ndoa zao na mahusiano yao.
Makaburi mengine ni la Darwesh aliyekuwa kiongozi wa mstari wa mbele kwenye mapambano ya kueneza dini ya Kiislamu na kaburi la kiongozi wa dini ya Kiislam Sheikh Ali bin Jumaa, ambaye alizaliwa mwaka 1215 na kufariki 1270.
Kaburi lingine ni la Sharifa lililojengwa kama nyumba na pembeni likiwa limezungukwa na makaburi ya watoto watatu waliomsindikiza kwa kipindi hicho.
Vivutio hivyo vimekuwa vikiongeza pato la taifa baada ya watalii wa ndani na nje kutembelea na kujionea historia ya Tanzania .
Viingilio hivyo kwa watalii hutozwa Sh. 13,000 kwa wanafunzi hadi Sh. 27,000 kwa watu wazima .
Aidha kwa watalii wa ndani hutozwa Sh. 1,000.
Moja ya Sera ya mali kale ni ukarabati wa mali hizo ambayo inatamka kurejesha sura, usanifu wa mali kale zilizochakaa au kuharibika kutokana na shughuli za kibinadamu au nguvu za asili kama mvua, upepo, tetemeko la ardhi kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya hifadhi.
Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Urithi wa Utamaduni, Digna Tillya, alisema changamoto kubwa inayowakabili ni baadhi ya watu huyatumia majengo ya kihistoria kuwa ya kibiashara.
Tillya alisema majengo ya kihistoria hayakutakiwa kubadilishwa kuwa ya kibiashara kama watu wengine wanavyofanya kwani yaliachwa kwa makusudi ya utamaduni. “Baadhi ya majengo yapo kwa wadau sasa hawa wamekuwa wakiyabadilisha na wengine kujenga kwa ajili ya biashara bila kutoa taarifa,” alisema.
Alisema majengo ya kale yaliyo katika maeneo ya kidini yamekuwa yakihifadhiwa vizuri kulinganisha na mengine yaliyopo kwa wadau wengine .
Tillya alisema serikali inamiliki vituo 16 ambavyo vinasimamiwa na Idara ya Mambo ya Kale.
Alisema katika vituo hivyo wanahakikisha kunakuwepo na mahitaji yote muhimu kwa watalii ikiwamo huduma ya kompyuta, ofisi, ukumbi, pamoja na magofu kuimarishwa.
Alisema tayari wamefanya maboresho makubwa katika vituo vinne vikiwamo vya Isimila, Kalenga, Ujiji na Kilwa Kisiwani.
Hata hivyo, alisema kwa mwaka huu mkakati wao ni kuboresha kituo cha Amboni kilichopo Tanga na Mbozi kilichopo Mbeya, viwe katika ubora ili watalii waweze kufurahia huduma zao.
Akizungumzia eneo la Kaole, Bagamoyo alisema tayari wamelifanyia maboresho na kwa sasa wanajipanga kuimarisha mipaka ya eneo hilo. Alisema maboresho ya maeneo ya kihistoria yanakwenda kwa awamu katika eneo hilo na kwamba katika bajeti ya mwaka ujao watatengeneza sehemu ya kutolea maelezo kwa wageni.
Tillya alisema ukarabati wa majengo unagharibu kiasi kikubwa cha fedha na wakati mwingine jengo moja linagharimu Sh. milioni 50 hadi Sh. 100
.
CHANZO: NIPASHEa
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment