Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
February 22, 2015
Makazi ya balozi wa Iran nchini Libya yashambuliwa
Miripuko miwili imejiri karibu na nyumba ya balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Tripoli, Libya.
Habari zinaeleza kuwa, miripuko hiyo iliyotokea kwa kupishana kwa dakika chache mchana wa leo, ilikuwa imemkusudia balozi wa Iran nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, baada ya shambulizi la kwanza, bomu la pili lililokuwa limetegwa ndani ya pipa la taka, liliripuka karibu na eneo kulipotokea mripuko wa kwanza.
Askari maalumu wa libya wamefanikiwa kugundua mada nyingine za miripuko zilizokuwa zimetegwa karibu na eneo hilo na kuzitegua. Tayari kundi la kitakfiri la Daesh limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo yamejiri bila mtu yeyote kujeruhiwa .
Inaelezewa kuwa, hujuma hiyo ambayo haikufanikiwa imejiri huku balozi wa Iran akiwa hayupo mjini Tripol, kwakuwa amekuwa akifanya safari za mara kadhaa za kutoka nje ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika .
Serikali ya Iran kupitia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hii, Bi Marziye Afkham, imelaani hujuma hiyo na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, milipuko hiyo imetokana na mabomu ya kutupwa kwa mkono. Kwengineko, msemaji wa jeshi la Libya ameitaja Qatar kuwa ni mdoli ulio ndani ya mkono wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA.
Ahmad al-Mismari, amekosoa vikali miamala mibaya ya Qatar kutokana na njama inazozifanyatekeleza dhidi ya nchi nyingine za Kiislamu na Kiarabu .
Al-Mismari ameongeza kuwa, Walibya kamwe hawatosahau dhuluma iliyofanywa na serikali ya Doha dhidi ya nchi yao na kusisitiza kuwa, Qatar ni mtekelezaji wa njama za Shirika la Kijasusi la Marekani CIA .
Hii ni katika hali ambayo Alkhamisi iliyopita, Jenerali Khalifa Haftar ambaye kwa sasa anaongoza operesheni zilizopewa jina la 'Karamat' dhidi ya makundi ya kigaidi na kitakfiri nchini Libya, alilaani vikali uungaji mkono wa Qatar na Uturuki kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri likiwemo la Daesh dhidi ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment