Wapiganaji wa kundi la Islamic state wavunja sanamu nchini Iraq


Wapiganaji wa Islamic state wamedaiwa kuvunja sanamu katika makavazi ya Mosul nchini Iraq .
Wapiganaji wa Islamic State wametoa kanda ya video inayowaonyesha wakivunja sanamu ndani ya makavazi katika mji wa Mosul nchini Iraq .


Video hiyo inaonyesha wanaume kadhaa wakiwa katika chumba kimoja cha makavazi ya kitaifa wakiangusha na kuharibu sanamu ziliko ndani .

Moja baada ya nyingine sanamu hizo zilizoundwa kwa njia maalum, zilirushwa na kutapakaa kila mahala.

Kisha wanaharibu sakafu na kisha sanamu za watu walioshika visu zikigongwa na kuharibiwa kabisa.

Miongoni mwa sanamu zilizoharibiwa ni pamoja na sanamu ya fahali iliyotengenezwa karne ya tisa kabla ya kuja kwa yesu kristu.
CHANZO .BBCA

Comments