Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Labels
event
news
February 21, 2015
Yamkini Misri ikafanya mashambulio ya anga Gaza
Makundi ya muqawama ya Palestina yamesema yametiwa wasiwasi na taarifa za uwezekano wa jeshi la Misri kufanya mashambulio ya anga katika Ukanda wa Gaza .
Vyombo vya habari vya Misri vimekuwa vikilichochea jeshi la nchi hiyo kuanzisha mashambulio ya anga dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa madai kwamba watu wenye silaha wamekuwa wakipenya na kuingia eneo la peninsula ya Sinai la Misri kutokea Ukanda wa Gaza, suala ambalo limeyatia wasiwasi makundi ya muqawama ya Palestina.
Kufuatia kuuliwa raia 21 wa Misri nchini Libya, tangu siku kadhaa nyuma ndege za kivita za jeshi la Misri zimekuwa zikiyashambulia maeneo ya kaskazini mwa Libya hususan mji wa Darna kwa sababu serikali ya Cairo inaitakidi kuwa magaidi wanaoendesha harakati zao ndani ya ardhi ya Libya watahatarisha usalama wa Misri.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari kuna uwezekano wa kukaririwa hatua hiyo dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa sababu vyombo vya habari vya Misri vinadai kwamba watu wenye silaha wamekuwa wakiingia ndani ya peninsula ya Sinai kutokea Gaza na kuwaua askari wa Misri.
Kwa mujibu wa duru za habari kuna uwezekano mkubwa wa jeshi la anga la Misri kushambulia ngome za brigedi za Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama ya Palestina HAMAS kwa sababu hivi karibuni vyombo vya mahakama vya Misri vililitangaza tawi hilo la kijeshi la Hamas kuwa ni kundi la kigaidi.
Kupaa ndege za uchunguzi za jeshi la Misri kwenye anga ya maeneo ya kusini mwa Ukanda wa Gaza hususan miji ya Rafah na Khan Yunes ambako kumeanza kufanyika tangu mwaka uliopita wa 2014 hadi sasa kumezidisha uwezekano wa kufanyika mashambulio ya anga ya Misri dhidi ya eneo la Gaza huko Palestina…
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment