Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Labels
event
news
April 29, 2015
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morgoro apewa siku mbili na Chadema kuwaachia watuhumiwa kabla balaa halijaanza.
.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani hapa, kimempa muda wa siku mbili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, kuwaachia watu 20 waliokamatwa kwa tuhuma za kumjeruhi askari polisi F 3328 Koplo Ramadhani, vinginevyo wataitisha maandamano.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Morogoro, James Mkude, alisema kitendo cha polisi kuvamia eneo la Mindu na kukamata watu ambao walikuwa katika maeneo hayo bila kuchunguza kama walihusika ama hawajahusika katika tukio hilo hakikubaliki.
Alisema Chadema haitetei uhalifu wa aina yoyote ile, lakini Jeshi la Polisi lilipaswa kuwatuma makachero wake katika eneo hilo kwenda kufanya uchunguzi kubaini waliohusika na tukio hilo na siyo kukamata kila mtu waliyemkuta na kuwaweka ndani pasipo kuwapa dhamana au kuwafikisha mahakamani.
Alisema endapo waliokamatwa hawataachiwa au kufikishwa mahakamani, Chadema itafanya maandamano makubwa ikiwamo kushirikisha wenye bodaboda ambao askari hao wamekuwa wakiwaonea na kwenda katika makao makuu ya polisi mkoa kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa hao.
Wiki iliyopita askari huyo anayeendesha pikipiki ya polisi maarufu ‘Polisi wa Tigo” akiwa kazini alijeruhiwa na watu wasiojulikana baada ya kupigwa na kitu butu kichwani wakati akitaka kumkamata kijana wa bodaboda aliyekuwa akimkimbia.
Kijana huyo wa bodaboda wakati akijaribu kukimbia aligongana na gari lililokuwa karibu na polisi huyo alipofika alipigwa na kitu kichwani na kisha watu hao kuchukua pikipiki ya bodaboda kwa lengo la kuificha.
Pia unaweza kujipatia habari na matukio mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kulike page yetu katika ukurasa wetu wa facebook www/facebook.cm/jamiileo tz.
CHANZO: NIPASHE
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment