Korea Kaskazini yaua maafisa serikalini
Shirika la kiinteligensia la Korea
kusini linasema utawala wa Korea kaskazini ,mwaka huu, umewauwa watu
waliokuwa na nyadhIfa za juu wapatao 15 , wanaodhaniwa kuwa wapinzani wa
utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un, kama njia ya kunyamazisha
upinzani nchi humo.
Habari hizi zilitokea wakati shirika hilo la kiintelijensia lilipozungumza na kundi la watunga sheria wa huko Korea Kusini.
Korea kazkazini haijatoa kauli yoyote kuhusiana na madai hayo lakini uongozi wa nchi hiyo umewahi kuwauwa baadhi ya wapinzani wao.
CHANZO BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment