Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Labels
event
news
religion
April 29, 2015
Makamu wa Rais wa baraza la maskofu afunguka asema Watanzania mawakala wa ugaidi
Pichani ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Seveline Niwemugizi
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Seveline Niwemugizi, amesema baadhi ya Watanzania wanafadhili vitendo vya kigaidi vinavyoendelea kutokea duniani.
Kauli ya Askofu Niwemugizi ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Rulenge, imefuatia taarifa za Mtanzania, Rashid Charles Mberesero (20), kukamatwa kwa kuhusishwa na shambulizi la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya na kusababisha mauaji ya wanafunzi 148. Askofu Niwemugizi alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifadhili vitendo vya ugaidi na vita takatifu, ama kwa kujua au kutojua.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera katika mafunzo maalumu ya elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu mapungufu yaliyomo kwenye katiba inayo pendekezwa kabla ya kuipigia kura.
“Napenda kuwatahadharisha sana Watanzania...wengi wetu wamekuwa wakifadhili ugaidi na vita takatifu, lakini baadhi yao hufadhili kwa kutojua na wengine kufahamu wanachokifanya kwa sababu ni mkakati wa muda mrefu ulioandaliwa kwa lengo maalumu,” alisema Askofu Niwemugizi.
“Ninasema haya siyo kwa bahati mbaya, umefanyika uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha undani wa maneno haya...kama mimi kuna kitu ninakielewa na nikakaa nacho kimya pasipo kuwataarifu nitakuwa ninafanya dhambi mbele ya Mungu wetu aliyeniagiza kuwachunga kondoo wake,” alisema.
Pia unaweza kujipatia habari na matukio mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kulike page yetu katika ukurasa wetu wa facebook www/facebook.cm/jamiileo tz
CHANZO: NIPASHE
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment