Skip to main content
Search
Search This Blog
JAMII LEO
HABARI, MICHEZO, MATUKIO, ,MAKALA ,BURUDANI ,DINI ,VIPINDI VYA REDIO/TV
Share
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Labels
habari
makala
May 03, 2016
WAANDISHI WA HABARI ZINDUKENI ACHENI NJAA
Na: Mwandishi wa Jamii LeoTz
Wapo baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya mikoa mbalimbali hapa nchini hufanya kazi kwa kujitolea eti kwa matumaini ya kuajiriwa na wengine hupenda rushwa na kufukuzana na bahasha za kaki katika makongamano , warsha ,semina , mahafali kila mawio na machweo .
Hakika hawa ndio wanaoishusha tasnia hii ya habari na kuonekana kazi isiyolipa au ilikosa dira , hapa jijini Arusha kuna redio mbalimbali ambazo sitapenda kuzitaja mjina yake kutokana na kauli za mameneja wa redio hizo kuwakera wanahabari wengi wa jiji hili na pia redio za mikoa mingine , na sio redio tu ! hata magazeti na runinga unapoenda kuomba ajira huambiwa ujitolee kwanza kwa miezi kadhaa ndipo uajiriwe.
Huu umegeuka kuwa mchezo mchafu kwa mameneja na viongozi mbalimbali wa vyombo hivyo vya habari , mfano kuna rafiki yangu mmoja ambaye ni mwandishi wa makala za uchunguzi aliwahi kuniambia kuwa kuna waandishi wa habari walijitolea kufanya kazi katika redio ya Country fm ya mkoani Iringa yapata miezi nane na hata ajira hawajapata na viongozi wa redio hiyo hawana matumaini ya kuwaajiri angali wanautambua na kuuhitaji mchango wao.
Hakika haya ni matokeo ya uwoga na ufinyu wa mawazo nyie ni kioo cha jamii, lakini mmekosa umakini na fikra mbadala
,mnatumia pesa binafsi kutafuta habari
,kula na mahitaji mengine huku mkifanya kazi kupita kiasi hakuna marupurupu wala" bonansi" , kuna redio moja hapa Arusha
ambayo imebeba jina la jiji hili waandishi wake wote wanajitolea yaani hawalipwi.
Usishangae hiyo ndio hali halisi , miaka ya nyuma nikiwa nafanya kazi Redio Nuur FM ya mkoani Tanga , siku moja nilipata taarifa kuwa Mheshimiwa Harrison Mwakyembe anakujakukagua bandari basi nami nikachukua vitendea kazi vyangu ikiwemo kinasa sauti na pia nikachukua kamera yangu kwa kuwa nilikuwa kipindi hicho nimeanzisha blogi yangu ya habari na matukio ili nami nikashuhudie ziara hiyo ya Mwakyembe ya ukaguzi wa bandari kweli nilifika mapema kabla mheshimiwa hajafika nikakuta waandishi wengine akiwemo Salmu Mohamed wa gazeti la Mwananchi , Wiliam Mngazija wa ITV , braza Mbonea wa Jambo leo na wengine ambao sitaweza kuwataja kwa leo ila alikuwepo mwandishi mmoja wa Brezee fm redio namkumbuka kwa jina moja la Agness aliponiona nimefika tu! Akaanza kuniuliza umekuja unamwaliko? …..
nikamwambia sina …. akaniambia basi huwezi pata bahasha nikahamaki kwanza !!!!
…. nikamuuliza na mimi wewe umefata bahasha au kujakuandika habari ….. akanijibu vyote kwa pamoja halafu akaendelea kusema "mshahara wenyewe hakuna ni vijiposho tu
sasa nyingine unakaa takribani miezi mitano posho wenyewe
hujapata wazani nitaishije"?alisema .
Kwakuwa marehemu baba yangu alinifundisha msemo kuwa "mtu mwerevu yamtosheleza ishara" kwakuwa nami ni miongoni mwa watu waelevu sio kwamba na jisifia hapana nikutokana na jamii ninayoishi nayo na hata mmoja wa wakufunzi wangu aliwahikuniambia hilo , nikaelewa kuwa Yule mwandishi hadi kufikia kusema vile inaonesha halipwi nikama anajitolea vile katika hiyo redio ndio maana akaniambia siwezi pata bahasha maana yangu ya kukuelezea tukio hili ni dhahiri kuwa mwandishi huyu anaona kwamba hiyo bahasha yenye elfu ishirini ndio itamtatulia matatizo yake .
Ndugu zangu wanahabari msiwe wepesi wakuandika shida za waalimu na madaktari
tu bali nanyie mjikumbuke , embu zindukeni na muache hizo njaa , tambueni thamani yenu hakuna asiye na shida ila kujionesha unanjaa kupita kiasi ni uzuzu tena na ubwege kabisa wakutojitambua .
Leo nikiuliza swali ni nani rais wa Marekani ? wengi mtajibu
Obama ama pia nikiuliza nini kinachoendelea huko Marekani? kwa sasa mtanijibu kuna mchakato wa kampeni za uchaguzi wa rais na David Trampy kasema akipita Waafrika watarudi kwao au nani rais watanzania wachache watamsahau.
Lakini swali mmejuaje? Jibu ni rahisi tena sana "vyombo vya habari vilisema" alisema na kuandika ni nani ni "huyu mwandishi asiyejua thamani yake " kama unabisha maliza wiki moja tu bila kusikiliza redio ,wala kutazama TV na kusoma gazeti pia kuperuzi internet , hakika nakwambia utajihisi upo gizani.
Ukitambua thamani yako utadai haki yako ,utatetea na kuitunza nami leo nawaambia
" wanahabari zindukeni acheni njaa" .
Msikubali kujitolea na kama inabidi basi andikishianeni mkataba wa muda wa kujitolea ili baada ya muda wa mkataba kuisha uajiriwe na tena mkubaliane kiwango cha mshahara ili msije mkawa kama marafiki zangu wa redio Fulani hapa Arusha wanaoelekea kumaliza miaka kwa kujitolea huku wakiliwazwa kwa maneno machafu na ya "ugwadu" ya bado tunakuangalia , eti meneja kasafiri , ila mimi naamini na nitaendelea kuamini kuwa tathnia hii bila kujitolea inawezekana.
Kama waandishi wote wahabari hapa nchini watakataa kujitolea wanapoambiwa wajitolee wanapoomba kazi
ni dhahiri kwamba kutakuwa na hitaji la wafanyakazi na nyie ndio mtakao ajiriwa, mfano hii Redio ya Arusha One inayosemekana
waandishi wake wote wanajitolea kama wafanyakazi wote wa redio hiyo wakifanya hivyo unadhani mmiliki atafunga kituo chake ? la hasha.
Lakini hamtawezafanikiwa kama hamtatengeneza umoja na kuwa na msimamo hii inasaidia kuepuka matokeo ya ule msemo
" wewe ukisusa sisi wenzio twala"
Pia ewe mwandishi uliyejitolea kwa muda sasa na hakuna hata matumaini ya kuajiriwa , usikate tama bali kaa chini keti kwa makini , tumia akili uliyopewa na Mungu bila uvivu wala papara ,tafuta ubunifu wa kipindi au vipindi kisha fanya siri yako anza kutafuta wadhamini ukishapata wadhamini , fedha kidogo lipia muda wa kipindi kuruka hewani kisha chenchi tia mfukoni kama anavyofanya mwandishi Issack Mwacha ambaye ametumia ubunifu wake baada ya kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari akaandaa kipindi chake cha kilimo akatafuta wadhamini na sasa kipindi chake kinaruka redio Maria kila siku ya jumapili kuanzia saa tatu au kama anavyofanya mzee wetu Jenerali Ulimwengu
.
Ama pia unaweza nunua vifaa kama kamera , vinasa sauti na laptop ukawa unauza habari na makala kwenye vyombo vya habari vyenye kulipa vizuri kama alivyokuwa akifanya marehemu Daud Mwangosi wa Channel Ten na marehemu Dotto Mzava au pia kama anavyofanya huyu mkufunzi wa Chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha Steven Mulaki ambaye ana kamera anazozikodisha kwa waandishi wa habari na wasio waandishi wa habari kwa ajili ya kufanyia kazi zao na wanamlipa.
Ubunifu wako kwa leo ndio maendeleo yako , hivi ewe ndugu yangu mwandishi wa habari humuoni Masudi anavyoingizaga mamilioni kupitia kipindi cha Maisha Plus pale TBC1 ,usidanganyike kwamba fani hii hailipi labla wewe ndio haulipi au bado hujajitambua na kutambua thamani yako ona wakina Millard Ayo na F.Kibonde wa Clouds fm wanavyoingiza mamilioni.
Yote katika yote simaanishi kujitolea ni dhambi ila cha msingi ni umakini , mfano huyu Millard Ayo aliwahi kujitolea kwenye redio moja ya dini hapa nchini lakini hicho hakikumzuia kutafuta ajira IPP MEDIA (ITV} na mwishowe kuhamia Clouds fm alipompaka sasa je? Angebweteka palepale alipokuwa redio ya dini kujitolea ,msikubali kufanywa ngazi
ZINDUKENI ACHENI NJAA
.
Comments
Popular Posts
March 12, 2013
USWAHILINI KUNA MAMBO ANGALIA PICHA HIZI ZA KANGA MOKO...SHETANI TOKAAAAAAAA!!!!!!
March 12, 2013
UNATAKA KUONA KANGA MOKO LAKI SI PESA...PICHA -- INYE NJE NJE...BALAA
Comments
Post a Comment